Kimenuka ila Dawa ya Madagascar Yashindwa Kudhibiti Maambukizi ya Corona
0
August 15, 2020
Hospitali nchini Madagascar zimekuwa zikikabiliana na ongezeko la maambukizi ya Covid-19, huku rais akiendelea kunadi dawa ya mitishamba anayodai ina uwezo wa kutibu ugonjwa wa Covid 19.
Visa vya maambukizi vimeongezeka mara nne zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita katika taifa hilo la kisiwani barani Afrika, huku zaidi ya watu 13,000 wakiambukizwa virusi na wengine na 162 kufariki kutokana na virusi vya corona, ambavyo vimesambaa karibu maeneo 22 ya nchi hiyo.
Licha ya ongezeka hilo la maambukizi, Rais Andry Rajoelina amesimama na dawa hiyo ya kienyeji inayofahamika kama Covid-Organics, ambayo ilizinduliwa kwa kishindo mwezi Aprili.
Ilitengenezwana Taasisi ya utafiti ya Madagascar kutokana na mmea wa artemisia – chanzo cha dawa inayotumiwa kutibu malaria na mimea mingine kutoka Madagascar.
Kinywaji hicho kilinadiwa kama tiba ambayo inaweza kuzuia na kutibu corona miezi minne iliyopita na imekuwa ikitumiwa na watoto shuleni.
Tags