Kiongozi wa upinzani Urusi awasili Ujerumani kupata matibabu



Msemaji wa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny amesema leo kuwa mwanasiasa huyo ameondolewa kutoka hospitali aliyokuwa anatibiwa katika mji wa Omsk huko Urusi na kupelekwa uwanja wa ndege ili kusafirishwa nje kwa matibabu. 


Ndege moja ya kibinafsi kutoka kwa shirika moja lisilo la kiserikali nchini Ujerumani ndiyo inayomsafirisha Navalny hadi mjini Berlin katika hospitali ya Charite kwa matibabu. 


Ndege hiyo ilifika mjini Omsk mapema jana ingawa madaktari wa Urusi walisema Navalny alikuwa katika hali mbaya sana na hakuweza kusafirishwa kwa wakati huo. 


Navalny alikuwa mgonjwa ghafla jana alipokuwa njiani kuelekea Moscow kutoka mji wa Siberia wa Tomsk na kusababisha ndege aliyokuwamo kutua ghafla. 


Madaktari walisema kwamba alikuwa katika hali mahututi akiwa amepoteza fahamu. 


Wasaidizi wake wanasema alipewa sumu iliyotiwa kwenye chai katika uwanja wa ndege wa Tomsk. Madaktari wa Urusi wamekanusha kupata sumu yoyote mwilini mwake na wanadai alifikia hali hiyo kwa kuwa kiwango chake cha sukari kilikuwa kimeshuka mno.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad