Kisa cha Mama wa Miaka 55 Aliyechomwa Hadi Kifo na Jamaa Wake


Mkasa huo ulitokea kufuatia mzozo wa ardhi

Mumewe mama huyo aliponea chupuchupu pamoja na mwanawe kwa majeraha mabaya

Familia hiyo ilikuwa imeishi katika shamba hilo kwa zaidi ya miaka 20

Waliomchoma ni jamaa wake aliokuwa akiishi nao awali

Kuishi kingi kuona mengi na kikulacho ki nguoni mwako. Wakazi wa eneo la Kyambuko kaunti ya Machakos wanaomboleza kifo cha mama mwenye umri wa miaka 55 aliyeuliwa kwa kuchomwa moto nyumbani kwake kufuatia mzozo wa ardhi.

Kulingana na jirani wa familia hiyo, Juliana Mwikali anadaiwa kuchomwa chumbani humo baada ya kufungwa mkono na miguu na hivyo kukosa uwezo wa kujiokoa.


‘’Tulimtoa akiwa amechomeka sana lakini mkono na mguu alikuwa amefungwa na binding wire… kwa hivo inaonekana walimchoma akiwa amefungwa,” alisema.

Kulingana na Jackson Makau mwanawe mama huyo, aliamshwa na mjomba na wapwa wake mwendo wa 5am na moja kwa moja wakaanza kumpiga.

“Wakanipiga ile mbaya sana tena wakanikata kata nikawa unconscious,”  Makau alisimulia.

Nelson ambaye ni mumewe mama huyo alishindwa kujieleza, kwa machozi alishangaa ni kwani watoto ambao aliwalea yeye nyumbani kwake walimgeukia na kuwa na lengo la kuimaliza familia yake.

Nelson anaeleza kuwa jamaa hao walimtafuta hadi Mtito Andei ambako ana boma jingine kabla kuelekea hadi Machakos kumuua mkewe.

Rhoda Khayi, naibu kamanda wa polisi katika kaunti hiyo ameeleza kuwa wanaume hao watano waliohusika katika kitendo hicho cha unyama tayari wamezuiliwa kusubiri kufikishwa mahakamani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad