Serikali ya Lebanon imesema kuwa mlipuko mkubwa ulioteteresha maeneo kadhaa ya mji wa Beirut umesababishwa na tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate iliyokuwa kwenye bandari ya mji huo.
MV Rhosus iliwasili bandari ya Beirut mwaka 3013 ikiwa imebeba tani 2,750 za kemikali ammonium nitrate
Watu wameonesha ghadhabu zao na kutoamini kuwa kiasi hicho kikubwa cha kemikali hatari iliwekwa kwenye ghala bila kuzingatia hatua zozote za usalama kwa zaidi ya miaka sita, kwenye eneo hilo ambalo liko karibu sana na eneo la katikati ya mji.
Serikali haijaeleza kemikali hiyo ilipotoka, lakini kiasi hicho hicho cha kemikali kiliwasili Beirut mwezi Novemba mwaka 2013 katika meli ya mizigo ya iliyokuwa na bendera ya Moldova, MV Rhosus.
Chombo hicho kinachomilikiwa na Urusi kilianza safari mwezi Septemba kutoka Batumi, Georgia kwenda Beira, Msumbiji.
Ilikuwa imebeba tani 2,750 za ammonium nitrate, ambayo huwa katika muundo wa madonge madogo madogo ambayo hutumika kutengeneza mbolea lakini pia inaweza kuchanganywa na mafuta kutengeneza vilipuzi kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini na katika sekta ya ujenzi.
Wakati ikisifiri kupitia mashariki mwa Mediterranea, MV Rhosus ilipata ”tatizo la kiufundi” na ikalazimika kutia nanga bandari ya Beirut, kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 iliyoandikwa na mwanasheria wa Lebanon aliyewawakilisha wafanyakazi wa meli hiyo.
Meli hiyo ilifanyiwa uchunguzi na maafisa wa bandari na ”kuzuiwa kufanya safari”, mawakili walisema. Sehemu kubwa ya wafanyakazi wake walirudishwa makwao, isipokuwa nahodha wa meli Mrusi, Boris Prokoshev, na wengine watatu walioripotiwa kuwa raia wa Ukraine.
Bwana Prokoshev aliliambia shirika la habari la Reuters siku ya Alhamisi kuwa meli hiyo ilikuwa inavuja, na kuwa ilipelekwa Beirut na mmiliki wake kwa ajiliya kubeba mzigo mwingine zaidi kwa sababu ya changamoto za kifedha.
Hatahivyo, wafanyakazi wa meli hiyo hawakuweza kubeba mzigo huo , na mmiliki aliposhindwa kulipa ada ya bandarini, mamlaka ya Lebanon iliizuia meli hiyo, alisema.
Muda mfupi baadae, MV Rhosus ”ilitelekezwa na wamiliki wake.
Muda kidogo baadae, MV Rhosus “ilitelekezwa na wamiliki wake kuonesha wasiwasi kuwa hawahitaji tena mzigo”, kulingana na wanasheria.
Wakati huo huo, bado wafanyakazi walikuwa wamezuiwa kwenye chombo hicho walikuwa wakikosa chakula na mahitaji mengine. Mawakili hao walisema waliomba kwa Jaji wa Masuala ya dharura huko Beirut atoe amri ya kuwaruhusu warudi nyumbani, wakisisitiza “hatari ambayo wafanyakazi walikuwa wakikabiliana nayo kwa kuzingatia” hatari “ya shehena ya mizigo” kwenye meli.Boris Prokoshev (Kulia), nahodha wa MV Rhosus, na raia wa Botswana Boris Musinchak wakiwa kando ya meli iliyobeba shehena ya kimikali ya ammonium nitrate
Hatimaye Jaji alikubali kuruhusu wafanyakazi wa meli hiyo kushuka na mwaka 2014 mamlaka ya bandari ilihamisha kemikali ya ammonium nitrate na kuiweka katika ”ghala namba 12”, karibu na ghala la nafaka.
Mawakili walisema mzigo huo ulikuwa ”ukisubiri kupigwa mnada au kuharibiwa”.
”Mzigo huo ulikuwa wenye uwezo wa kulipuka. Ndio maana ulibaki ndani ya meli tulipokuwa huko…,” alisema bwana Prokoshev.
Aliongeza: ”Nina masikitiko kwa watu (waliopoteza maisha au kujeruhiwa na mlipuko). Lakini mamlaka nchini humo zinapaswa kuadhibiwa. Hawakuujali mzigo huo kabisa.”Transparent line
Mkurugenzi Mtendaji wa bandari, Hassan Koraytem, na Mkurugenzi wa mamlaka za mapato, Badri Daher, kwa pamoja walisema siku ya Jumatano kuwa wao na maafisa wengine walikuwa wakitahadharisha mahakama kuhusu hatari ya kuhifadhi kemikali ya ammonium nitrate na uhitaji wa kuiondoa.
Nyaraka zilizosambaa mtandaoni zilionesha barua za maafisa hao kwenda kwa jaji wa masuala ya dharura mjini Beirut wakitaka muongozo jinsi ya kuuza au kuharibu ombi ambalo lilipelekwa karibu mara sita tangu mwaka 2014 mpaka mwaka 2017.
Bwana Koraytem alikiambia chombo cha habari cha nchini humo OTV kuwa idara ya usalama pia ilituma barua za tahadhari.
Waziri wa ujenzi Michel Nijjar, ambaye ameingia madarakani mwanzoni mwa mwaka huu, aliiambia Al Jazeera kwamba alibaini uwepo wa kemikali ya ammonium nitrate mwishoni mwa mwezi Julai na kuwa alizungumza na bwana Koraytem kuhusu jambo hilo siku ya Jumatatu.
Mlipuko katika bandari ya Beirut uliua watu takribani 137 na kuwajeruhi watu karibu 5,000, wengine wakiwa hawajulikani walipo.Athari za mlipuko mjini Beirut
Rais Michel Aoun amesema kuwa kushindwa kushughulikia mzigo wa meli ya Rhosus ”hakukubaliki” na kuahidi ”kuwashughulikia waliohusika na katika kitendo cha kizembe cha kupuuza na kuwaadhibu vikali.”
Serikali imeamuru maafisa waliohusika na kuhifadhi au kuongoza shughuli za kukamata mzigo wa shehena ya kemikali ya ammonium nitrate.