Kiwanda bandia cha mvinyo chakutwa ndani ya chuo kikuu, Zambia


Mamlaka ya Zambia,katika mji mkuu wa Lusaka imebaini kuwepo kwa kiwanda cha mvivyo ambacho kilikuwa kinaendeshwa kinyume na sheria ndani ya chuo kikuu kimoja nchini humo, mtandao wa Lusaka Times umeripoti.


Maofisa wa afya walitoa taarifa baada ya kupokea malalamiko kutoka uongozi wa chuo cha Evelyn Hone zilizodai kuwepo kwa harufu mbaya iliyokuwa ikitokea upate wa mgahawa wa shule.



Baada ya ufuatiliaji zaidi, maofisa hao waligundua kuwa hatua zote za utengenezaji wa mvinyo zilikuwa zikifanyika katika eneo moja ikiwa ni pamoja na utengenezaji chupa na pombe yenyewe.



Mmiliki wa kiwanda hicho alisema ameshindwa kupata kibali cha kutengeneza na kusambaza pombe hiyo hali iliyomlazimu kuendesha bila usajili.



Bado haijawekwa wazi iwapo mmiliki wa kiwanda hicho ndiye mmiliki wa mgahawa huo pia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad