Kocha Mpya Yanga Mzigoni Wiki Ijayo


UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umefunguka kuwa unatarajia kumtambulisha rasmi kocha wao mkuu mapema wiki ijayo tayari kuanza kazi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo kilichoanza mazoezi mwanzoni mwa wiki hii.

Yanga ipo katika mchakato wa mwisho wa kumpata kocha mkuu baada ya kuachana na Mbelgiji, Luc Eymael ambaye alitumuliwa hivi karibuni.

Taarifa ambazo Spoti Xtra imezipata kutoka Yanga, zinasema kuwa, Mshindo Msolla ambaye ni mwenyekiti wa klabu hiyo, mapema wiki ijayo atamuweka wazi kocha huyo baada ya mchakato wa kumsaka kukamilika.

“Kocha mkuu anatarajia kutoka nje ya nchi na msaidizi wake ni mzawa, tayari tumemalizana nao na wiki ijayo tutawatambulisha rasmi na kuanza majukumu ya kukinoa kikosi.
“Kuna vitu ambavyo vinaendelea kukamilishwa kabla ya kutangazwa kwa kocha mpya na benchi lake la ufundi, huku kikosi kikitarajiwa kuingia kambini kuanzia Jumatatu,” alisema mtoa taarifa huyo.
Tangu kuachana na Eymael, Yanga imekuwa ikihusishwa na makocha wengi wanaoitaka nafasi hiyo wakiwemo makocha wa zamani wa timu hiyo, Mholanzi, Hans Pluijm na Mbrazil, Marcio Maximo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad