Kocha Mrundi Atua Yanga, Aanza Kazi Fasta




ALIYEWAHI kuwa kipa wa Azam FC, Vladimir Niyonkuru raia wa Burundi aliwasili rasmi nchini Tanzania, juzi mchana tayari kwa kuanza kazi ya kuwanoa makipa wa Yanga kuelekea msimu ujao wa 2020/21.

Yanga ambayo kwa sasa ipo katika mkakati wa kujijenga upya kufuatia kufumua benchi lake lote la ufundi baada ya msimu wa 2019/20 kufikia tamati, ilimuondoa aliyekuwa kocha wake, Luc Eymael raia wa Ubelgiji baada ya kutoa lugha ya kibaguzi, hivyo ipo mbioni kusaka kocha mpya wa kuziba pengo lake kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuanza Septemba sita.

Taarifa ambazo Championi Ijumaa ilizipata kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, kocha huyo aliwasili juzi na kisha jana Alhamisi gazeti hili likamshuhudia akianza kazi kwa kutoa malekezo katika mazoezi ya timu yake hiyo mpya.

Yanga ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Ubungo jijini Dar, na kocha huyo alikuwa bize kuwanoa makipa wa timu yake.

“Tumeshafanikiwa kumpata kocha wa makipa Niyonkuru raia wa Burundi ameshaanza kazi na kinachobakia hivi sasa ni kumtangaza kocha mkuu mambo yakishakamilika.

“Mambo yetu yameonekana kuyumba kumpata kocha mpya kutokana na Virusi vya Corona, hivyo kila kitu kinakuwa kigumu lakini mwisho wa siku Mungu atasaidia na tutamtangaza kocha,” alisema mtoa taarifa huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad