Kupatana na Kajala Siwezi Moyo Wangu Bado- Wema Sepetu



Ikiwa ni siku moja baada ya mrembo Wema Sepetu kupatana na rafiki yake Aunty ezekiel, mashabiki sasa wamtaka amgeukie na Kajala ambapo mwenyewe amefunguka kuhusu hilo.


Wema na Aunt walikuwa wamegombana kwa miezi kadhaa lakini jana Alhamisi Agosti 6, 2020 walionesha kuzika tofauti zao baada ya kupatanishwa na Petitman Wakuache.


Akihojiwa leo Ijumaa Agosti 7, 2020 na Clouds Fm, Wema amesema yeye kama binadamu kuna ugomvi mkubwa na mdogo, lakini kwa Kajala anauweka katika ugomvi mkubwa.

Kutokana na hilo, amesema hataki unafiki na hayupo tayari kwa sasa kupatana na Kajala isipokuwa anamuachia Mwenyezi Mungu.

“Kupatanishwa kwetu hakujaanza jana wala leo, hata Steve Nyerere alishajitahidi kutafuta suluhu kuhusu hilo, lakini hajafanikiwa hadi leo, hivyo katika hili naomba niachwe kwanza sipo tayari kwa sasa,” amesema @wemasepetu anayetesa na tamthiliya ya Karma kwa sasa.


Alipoulizwa kama ikatokea #Kajala akahitaji wapatanishwe atakuwa yupo tayari, amesema hiyo ni yeye lakini kwa sasa aachwe kwanza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad