Maamuzi mazito ya Yanga dhidi ya Benard Morrison



Uongozi wa klabu ya Yanga umesema leo Agosti 24 unawasilisha shauri la mchezaji Benard Morrison katika mahakama ya uluhishi wa michezo (CAS) kutokana na kutoridhishwa na maamuzi yalitolewa na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji Agosti 12 mwaka huu.


Winga machachari Benard Morrison akisaini mkataba wa kuitumikia Simba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dr Mshindo Msola amesema wanapeleka shauri hilo ili kupata haki sababu uwepo wa mapungufu katika mkataba wa Morrison si sahihi kubatilisha mkataba huo.

"Uamuzi wetu wa kuwasilisha malalamiko yetu katika Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo CAS kuhusu Bernard Morrison uko palepale,  na leo tunawasilisha rasmi"..Dk Mshindo Msola Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga.

Kuhusu usajili Mwenyekiti Msola amewataka wanachama kuchangisha fedha kwa ajili ya usajili wa nafasi mbili za wachezaji wa kigeni ambapo pia Dr Msola amemtambulisha Senzo Masingiza kuwa mashauri wa klabu hiyo.

"Tumeona tumuongeze bwana Senzo Mbatha katika mchakato wa mabadiliko, kutokana na rekodi yake katika masuala ya soka, hivyo atakuwa mshauri kama walivyo La Liga na Sevilla na baada ya kukamilika ataendelea kutusimamia" - Dkt Mshindo Msolla, Mwenyekiti wa Yanga.

Katika kilele cha maadhamisho ya wiki ya Mwananchi Agosti 30 mwaka huu Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa  kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Aigle Noir kutoka nchini Burundi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad