Majadiliano na Urusi Kuhusu Chanjo ya Corona Yanaendelea – WHO
0
August 21, 2020
Shirika la Afya Duniani, WHO barani Ulaya limesema limeanza majadiliano na Urusi kujaribu kupata taarifa zaidi kuhusu chanjo ya ugonjwa wa COVID-19 ambayo imeidhinishwa na nchi hiyo hivi karibuni. Wiki iliyopita, Urusi ilikuwa nchi ya kwanza duniani kutoa ridhaa ya kutumika kwa chanjo ya virusi vya corona wakati Rais Vladmir Putin alipoiidhinisha chanjo hiyo.
Hata hivyo, chanjo hiyo bado haijafanyiwa majaribio yanayotakiwa ili iweze kuidhinishwa kutumika. Catherine Smallwood, afisa wa ngazi ya juu wa dharura wa WHO barani Ulaya amesema shirika hilo limeanza mazungumzo ya moja kwa moja na Urusi.
Smallwood amesema maafisa wa WHO wameanza kubadilishana taarifa kadhaa ambazo zinahitajika kufanyiwa tathmini na shirika hilo. Mkurugenzi wa WHO barani Ulaya, Dokta Hans Kluge amesema shirika hilo limefurahishwa na maendeleo ya chanjo hiyo, lakini kila chanjo lazima iwasilishwe kwenye hospitali zao kwa ajili ya majaribio.
Tags