JESHI la polisi mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limefanya operesheni maalum ya kudhibiti makosa ya jinai na kufanikiwa kuwaua majambazi wawili na kukamata silaha zao pump action na risasi kumi .
Jeshi la polisi lilipata taarifa za kiitelijensia kuwa kuna majambazi wamepanga kufanya tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha katika moja ya viwanda vilivyopo eneo la Zegereni ,Mlandizi.
Agost 7 mwaka huu ,jeshi hilo liliweka mtego na kufanikiwa kuwaona majambazi hao wakiwa watatu kwenye pikipik moja wakielekea eneo la viwanda.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Pwani ,Wankyo Nyigesa ,akithibitisha juu ya tukio hilo ameeleza, askari walipowasimamisha hawakusimama na jitihada za kuwafukuza zilianza mara moja ,askari walipowakaribia watu wawili waliruka kwenye pikpik na kuanza kukimbia huku wakirusha risasi kwa askari .
Walianza kurushiana risasi na majambazi hao ambapo walijeruhiwa na baadae walifariki wakiwa njiani wakipelekwa hospital.
Wankyo ameeleza,jambazi mmoja aliyekuwa dereva wa pikpiki amefanikiwa kukimbia na majambazi waliouawa ,miili yao imehifadhiwa hospital ya Tumbi .
Wakati huo huo jeshi hilo linawashikilia watu watatu waliohusika na wizi wa hydrolic pump ya gari mtambo wa kuchimbia mchanga yenye namba za usajili T.525 DFN aina ya Komasu yenye thamani ya milioni 15 Mali ya kampuni ya Yong Da comp.ltd ya Masaki Dar es salaam.
Wankyo amewataja watu hao kuwa ni Hamis Zaitun Janja 40, Saimon Chache 37 na Evance Kimaro miaka 28 ambao wamekiri kuhusika na wizi huo .