Makabiliano mapya yazuka Marekani baada ya kushambuliwa kwa Jacob Blake



Majumba na magari yamechomwa moto katika usiku wa pili wa maandamano kufuatia kupigwa risasi kwa mtu mweusi kwa jina Jacob Blake siku ya Jumpili.

Jacob Blake, 29, yupo katika hali nzuri baada ya kupigwa risasi mara kadhaa alipokuwa anafungua mlango kuingia ndani ya gari katika mji wa Kenosha.

Gavana Tony Evers amekitaka kikosi cha kitaifa kuwasaidia maafisa wa polisi.

Mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd huko Minnesota mwezi Mei yalisababisha maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi na unyanyasaji unaotekelezwa na polisi.

Maandamano kote nchini Marekani na miji mingi kimataifa yaliangazia jinsi Wamarekani weusi wanavyonyanyaswa na maafisa wa polisi hatua iliozua maswali mengi khusu ubaguzi katika jamii .

Kanda ya video kuhusu mauaji hayo ya Kenosha, iliochukuliwa barabarani na kusamabazwa katika mitandao ya kijamii, ilimuonesha Bwana Blake akitegemea gari huku afisa mmoja akivuta shati lake na milio ya risasi ikisikika.


Sheria ya kutotoka nje imewekwa mjini Kenosha kuanzia saa mbili usiku na itaendelea hadi saa moja alfajiri siku ya Jumanne- sheria hiyo hata hivyo imepuuzwa na waandamanaji


Ilianza kama ukumbusho kwa wengi katika miji na majiji nchini Marekani baada ya kifo cha George Floyd huku mamia ya vijana mjini Kenosha wakivunja amri ya kutotembea usiku na kukabiliana na polisi waliokuwa wamejipanga nje ya mahakama.


Maandamano hapa wakati huu, yanayohusu kutaka haki kwa Jacob Blake, awali yalizuiwa na kutawanywa kwa gesi ya kutoa machozi na mabomu ya kutoa sauti, lakini watu waliendelea.


Hata hivi sasa mapema asubuhi bado wanakabiliwa na maafisa wakiwa na ngao kuwazuia waandamanaji. ''Hatuondoki'', walikuwa wakiimba.


Katika mitaa iliyokuwa ikiwazunguka tuliona magari yakiwa yamechomwa moto, majengo yakiwa yameharibiwa na taa za mitaani zikiwa zimeangushwa.


Kijana mmoja muandamanaji aliniambia. '' Nimechoka kuwa na hofu ya kuuawa na polisi. Usiku huu watatusikiliza.''


Polisi na serikali wamesema nini?


Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Gavana Evers amesema ''ombi la kupata maafisa wa ulinzi ilikua ni kusaidia kusimamia sheria ''kulinda miundombinu'' na kuhakikisha kuwa watu wanaandamana kwa usalama.


Alisema kuwa anasambaza maafisa karibu 125 wa kulinda usalama Jumatatu usiku.


Mapema asubuhi baaadhi ya waandamanaji walijaribu kuingia kwenye jengo la usalama la mji wa Kenosha, wakitaka maafisa waliohusika katika tukio la kufyatua risasi wakamatwe.


Mlango ulivunjwa kabla ya maafisa kutumia dawa ya kupuliza yenye pilipili kusambaratisha kundi la watu.


Mamia ya watu pia waliandamana mpaka makao makuu ya polisi usiku wa Jumapili wakikemea tukio hilo.


Gavana Evers amekemea tukio hilo, akisema kuwa Bwana Blake hakuwa ''mtu wa kwanza kufyatuliwa risasi au kujeruhiwa au kuuawa mikononi mwa polisi.''


Lakini gavana huyo amekosolewa kutokana na kauli yake, mkuu wa polisi mjini Kenosha Pete Deates, amesema kuwa kauli ya Evers ''haikuwa ya kuwajibika'' na kusema kuwa watu wanapaswa kusubiri mpaka pale ukweli utakapojulikana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad