Mamia Waandamana Baada ya Askari Walevi Kuua Watu 13 DRC
0
August 01, 2020
Askari waliokuwa wamelewa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamemimina risasi na kuua watu 13 na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Mmoja wa wahanga anaripotiwa kuwa mtoto wa miaka miwili.
Mauaji hayo yalitokea usiku wa Alhamisi katika jimbo la Kivu kusini mashariki mwa nchi hiyo
Jeshi la Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo linawatafuta askari hao waliouwa watu 13, wakiwemo wanawake na watoto katika mji wa Uvira.
Makundi kadhaa ya wanajeshi pamoja na walinda amani wa Umoja wa mataifa wako katika mji huo ili kuwalinda raia.
Ni siku ya masikitiko makubwa katika fukwe za ziwa Tanganyika, kumekuwa na waandamanaji wenye hasira dhidi jeshi la Kongo katika mji wa Sange, tangu majira ya asubuhi eneo ambalo barabara nyingi zilikuwa zimefugwa.
Waandamanaji hao wanataka familia zilizoathirika kulipwa fidia na huduma za afya kwa wale waliojeruhiwa.
Jeshi limeiambia BBC kuwa askari wale walifanya tukio hilo kwa sababu walikuwa wamelewa na watafukuzwa jeshini na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Tukio hili limekuja wakati ambao mji huo bado ulikuwa unakabiliana na athari za mfuriko makubwa yaliyouwa watu 40 na wengine maelfu walipoteza makazi yao.
Tags