Marekani yaidhinisha matumizi ya dharura ya maji ya damu



Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA) imetoa idhini ya dharura ya matumizi ya maji maji ya damu kuwatibu wagonjwa wa corona.


Mfumo huo wa tiba unatumia maji hayo kutoka kwa watu waliopona ugonjwa huo, na tayari umewatibu watu zaidi ya 70,000 nchini Marekani.


Raid Donald Trump amesema tiba hiyo huenda ikapunguza idadi ya vifo kwa asilimia 35.


Amesema hayo siku moja baada ya kuishutumu FDA kwa kuweka vizuizi dhidi ya kusambazwa kwa chanjo na tiba zingine kwasababu za kisiasa.


Tangazo hilo limetolewa mkesha wa kangamano la kitaifa la champ cha Republican, ambapo Bw. Trump atazindua kampeini yake ya kugombea muhula wa pili madarakani.


"Nimekuwa nikitazamia kufanya hivi kwa muda mrefu," rais aliwaambia wanahabari siku ya Jumapili. "Nafurahia kutoa tangazo la kihistoria katika makabiliano yetu dhidi ya virusi vya China ambavyo itaokoa maisha ya watu wengi."


President Trump alisifu mfumo huo wa tiba kuwa imara na akawapongeza Wamarekani kwa kujitokeza kutoa masaada wa maji hayo ikiwa wamepona kutokana na Covid-19.


Mamlaka ya FDA awali ilisema kuwa utafiti umebaini kuwa maji ya damu [plasma] yana uwezo wa kupunguza idadi ya vifo na kuimarisha afya ya mgonjwa ikiwa atafanyiwa tiba hiyo siku tatu za kwanza baada ya kulazwa, japo majaribio zaidi yanahitajika kufanywa ili kuthibitisha uwezo wake.


Shirika hilo lilithibitisha kuwa ni salama kutumia mfumo huo wa tiba baada ya kufanya uchunguzi zaidi data zilizokusanywa miezi ya hivi karibuni.


Katika taarifa yake, iliongeza kuwa faida ya tiba hiyo inazidi hatari ya aina yoyote .


Lakini wataalamu kadhaa, akiwemo Anthony Fauci, mwanachama wa jopo kazi la White House kuhusu coronavirus, wametilia shaka utafiti huo kufikia sasa.


FDA tayari imeidhinisha wagonjwa wa corona waongezewe utegeli chini ya uangalizi maalum, hasa wale ambao wako hali mahututi ama wale wanaofanyiwa majaribio ya kimatibabu.


Katika ujumbe wa Twitter siku ya Jumamosi, rais Trump alisema "Kuna watu, ndani ya FDA ambao wamefanya kuwa vigumu kwa mashirika ya dawa kupata watu wa kufanyiwa majaribio ya chanjo na tiba zingine.


"Bilashaka, wanajaribu kuchelewesha matokeo hadi baada ya [uchaguzi wa urais wa Marekani]," aliongeza.


Mapema mwaka huu, Mamlaka hiyo ya udhibiti wa dawa iliidhinisha kwa dharura matumizi ya dawa ya remdesivir kama tiba ya corona .


Huku hayo yakijiri, taarifa katika gazeti la Financial Times zinaashiria kuwa White House inapania kutoa idhini ya dharura ya matumizi ya chanjo inayotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford na shirika kubwa la dawa la AstraZeneca, kabla ya uchaguzi wa urais wa Marekani Novemba tarehe tatu.


White House haijatoa tam polite kuhusiana na taarifa hiyo, lakini msemaji AstraZeneca ameliambia shirika la habari Reuters kwamba matokeo ya majaribio ya chanjo hiyo haitarajiwi kutolewa hadi baadae mwaka huu.


Zaidi ya watu 176,000 wamefariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19 tangu uliporipotiwa nchini Marekani, kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Karibu watu milioni 5.7 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona kote nchini humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad