IDARA ya Ushauri wa Afya ya Marekani imeitaja nchi ya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi salama ambazo wananchi wake (Wamarekani) wanaweza kuitembelea katika majira haya ya joto.
Taarifa iliyotolewa na idara hiyo na kutangazwa na kituo cha Televisheni cha CNN, imesema wananchi wake wanaweza kuitembelea Tanzania lakini wakifika lazima wafanye vipimo vya Covid-19 kabla ya kuendelea na shughuli zao.
Hivi karibuni Serikali ya Tanzania kupitia kwa Rais John Magufuli ilifungua milango kwa watalii kutoka nchi mbalimbali kuja kuitembelea na kwamba ugonjwa wa Covid-19 umedhibitiwa hapa nchini lakini ni vyema wananchi na wageni kuendelea kuchukua tahadhari.
Wamarekani wanaruhusiwa kuingia kwenye nchi hizi bila masharti:
Albania
Dominican Republic
Kosovo
Maldives
Mexico
North Macedonia
Serbia
Tunisia
Turkey
Wamarekani wanaruhusiwa kuingia kwenye nchi hizi kwa masharti ya kupima Covid-19.
Antigua and Barbuda
Aruba
Barbados
Belize
Bermuda
Cambodia
Croatia
Dominica
Ecuador
Egypt
French Polynesia
Ireland
Jamaica
Rwanda
St. Barts
St. Lucia
St. Maarten
St. Vincent and Grenadines
Tanzania
Turks and Caicos
Ukraine
United Arab Emirates
United Kingdom