Marekani Yatengeneza GARI Linalopaa Angani



HATIMAYE magari yenye kupaa yamewasili! Baada ya jitihada za kuunga mashine mbalimbali na kufanya majaribio kadhaa, Jeshi la Anga la Marekani, kwa kushirikiana na kampuni ya Lift Aircraft, wamefanya onyesho la gari la kwanza lenye uwezo wa kuondoka chini na kupaa moja kwa moja juu ambalo hutumia mota za umeme (eVTOL).


Onyesho la hilo gari hilo lililopewa jina la Hexa, limefanyika siku ileile ya kumbukumbu ambapo ndugu wawili wa Wright walipaisha ndege angani kwa mara ya kwanza miaka 112 iliyopita.

Tukio hilo lilienda sambamba na mpango wa kile kilichoitwa ukakamavu (Agility Prime) katika jeshi hilo, likimujuisha wabunifu, jamii mbalimbali na hata matukio yenye kulenga kuendeleza aina hiyo ya magari.

Pakua App ya Global kwenye Google Playstore, App Store. Utasoma Habari, Magazeti yote kutoka GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad