Marekani yawawawekea vikwazo raia wanne wa Uganda



Wazazi waliambiwa watoto watasomeshwa katika shule maalumuImage caption: Wazazi waliambiwa watoto watasomeshwa katika shule maalumu

Serikali ya Marekani imewasilisha kesi ya udanganyifu na usafirishaji haramu dhidi ya wale waliohusika mpango wa uasili wa watoto ambao walikuwa si yatima na kuwatoa kwa familia za Wamarekani.




kuwa Watoto wa Uganda walichukuliwa kutoka aktika familia zao kwa ahadi kuwa watasomeshwa katika shule maalumu nchini Marekani.




Badala yake walifikishwa mahakamani kama yatima kwa ajli ya kuasiliwa na Wamarekani.




Marekani imewawekea vikwazo raia wanne wa Uganda miongoni mwao majaji wawili kwa kuhusika katika biashara haramu ya kimataifa ya mfumo wa uasili.




Taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani iliyotolewa Jumatatu, inasema kuwa Jaji ya ngazi ya juu Wilson Musalu Musene na Mkuu wa zamani wa kitengo cha uhalifu wa kimataifa, Jaji mstaafu Moses Mukiibi walishiriki katika njama ambapo watoto wadogo walichukuliwa kutoka kwa familia zao na kukabidhiwa kwa mtandao haramu unaowaasili kwa njia za ufisadi kwa kusaidiwa na maafisa wa Uganda.




Hongo zinadaiwa kulipwa kwa majaji hao wawili ili wahalalishe kesi za watoto hao.




Mawakili wawili ambao pia wamewekewa vikwazo hivyoni , Dorah Mirembe na Patrick Ecobu ambao wanadaiwa kusaidia kutoa hongo kwa majaji wa Uganda na maafisa wengineili kuidhinisha mchakato wa kesi za uasili kinyume cha sheria. Vikwazo hivyo ni vya kifedha pamoja na kusafiri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad