Mbasha aishukuru serikali kwa kuwapatanisha na Mchomvu "Nilishamsamehe tangu usiku ule alionikosea"
0
August 18, 2020
Siku chache baada ya Mtanazaji wa Clouds FM Adam Mchomvu na muimbaji wa nyimbo za injili Emmanueli Mbasha kutofautiana katika tamasha la 'Uhuru kuna jambo' wote wamaliza tofauti zao.
Adamu alikuwa wa kwanza kuomba msamaha kwa rais pamoja na watu wote kwa ujumla naye Mbasha ameishukuru serikali kwa kuwapatanisha.
Kupitia akaunti ya instagramu ya Mbasha ameandika hii;
"Kwa Maslahi ya Taifa langu la Tanzania nikiwa kama balozi wa amani, napenda kumshukuru Rais wangu na baba yangu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, pamoja na msemaji Mkuu wa Serikali Dr Hassan Abbas pamoja na chama changu cha CCM kwa kuona tatizo lililojitokeza kati yangu na Adam Mchovu. Kwa kuonyesha kuheshimu hatua hii ya Serikali yangu pendwa ya Tanzania ya kunipatanisha na huyu kijana, napenda kuwahakikishia kuwa mimi nilishamsamehe tangu usiku ule alionikosea. Maana nikiwa kama kiongozi wa waimbaji wote wa nyimbo za injili nchini Tanzania nimeshika na kuizingatia miiko yote ya uongozi haswa katika upande wa imani yangu ya kikristo ambayo inatanguliza mbele msamaha pamoja na kuchukuliana. Moyoni mwangu sina kinyongo kabisa wala sina muda wa kutafuta kulipa kisasi kwa sababu biblia inasema, "Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote pamoja na huo utakatifu ambao hakuna awezae kumuona Mungu asipokuwa nao" (Waebrania 12:14).
Natamani sana tukio hili liwe fundisho kwa vijana wenzangu kwa kutokulipa ubaya kwa ubaya, bali tuushinde ubaya kwa kutenda wema... Naomba tumpe Rais Magufuli miaka mitano mingine ili aendelee kutunyoshea Nchi' BY @e.mbasha
Tags