Meninah Apewa Makavu Laivu "Anajirekodi Mwenyewe Alafu Anakuwa wa Kwanza Kukimbilia Polisi"



MSANII wa muziki, filamu na mshehereshaji maarufu Bongo, Meninah Attick, amepewa makavu laivu baada ya kuposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anafanyiwa masaji na mwanaume.

Meninah aliposti video hiyo akifanyiwa masaji na mwanaume asiyejulikana, jambo ambalo liliwakera wafuasi wake waliosema kwamba, anarudia yaleyale ya mwaka jana.

Baadhi ya wafuasi hao walimshambulia kwa kusema kuwa mambo mengine anajitakia mwenyewe.

“Huyu mwanamke sijui huwa hajielewi? Anajirekodi mwenyewe video zake halafu anakuwa wa kwanza kukimbilia Polisi na kuwaletea shida watu wengine,” aliandika mmoja wa wafuasi wake anajiita Saraatz.

Oktoba 10, mwaka jana, Meninah aliitwa na Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kuhusishwa na kosa la kusambaza video chafu kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo lilimuingiza matatani mwigizaji na komediani Burton Mwemba ‘Mwijaku’ ambaye mpaka sasa ana kesi ya Makosa ya Mtandao.

STORI: KHADIJA BAKARI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad