Mfahamu msanii Jay Z kiundani zaidi
0
June 05, 2022
Desemba 4, 1969 alizaliwa msanii wa hip hop na mfanyabiashara wa nchini Marekani maarufu Jay Z. Jina lake halisi ni Shawn Corey Carter.
Huyu ni mwanamuziki, rapa, mtunzi wa nyimbo, mwimbaji, prodyuza na mjasiriamali. Amekuwa akichukuliwa kuwa rapa wa zama zote. Alizaliwa katika kitongoji cha Brooklyn kilichopo New York City.
Wakati anasoma alisoma na marapa wengine Notorius B.I.G na Busta Rhymes. Jay Z alianza medani ya muziki baada ya kuanzisha lebo ya Roc-A-Fella Records mwaka 1995. Pia alishawahi kusimamia Def Jam Recordings. Baada ya lebo ya Roc-A-Fella Jay Z aliachia albamu mwaka uliofuata ya Reasonable Doubt.
Albamu hiyo ndiyo iliyoweka msingi wa maisha yake katika medani ya muziki. Jay Z alikuja kuachia albamu nyingine 12 ambazo kwa hakika zilipokelewa vizuri katika soko; ikiwamo ya The Blueprint ya mwaka 2001 na ile ya Black Album ya mwaka 2003. Jay Z alikuja kutoa albamu nyingine kwa ushirikiano na Kanye West na Beyonce Watch the Throne ya mwaka 2011 na Everything is Love ya 2018.
Nje ya masuala ya muziki Jay Z amejipatia mafanikio makubwa katika biashara. Mnamo mwaka 1999 alianzisha biashara ya nguo Rocawear. Mnamo mwaka 2003 alianzisha klabu ya The 40/40 na baadaye akaanzisha kampuni la burudani Roc Nation ambalo alilianzisha mwaka 2008.
Mnamo mwaka2015 alinunua kampuni ya mawasiliano la Norway maarufu Aspiro AB na baadaye akachukua umiliki wa huduma ya mtandao kupitia huduma ya Tidal ambayo ilizinduliwa mwaka 2014. Baada ya uzinduzi wa Tidal ukaiweka huduma hiyo ya online streaming katika nafasi ya tatu ulimwenguni.
Pamoja na kuwa na mafanikio yake makubwa ya kimuziki, Jay-Z anafahamika zaidi kwa kujihusisha na masuala ya ugomvi na baadhi ya wasanii wengine wa soko zima la rap, miongoni mwa ugomvi mkubwa uliokuwa unajulikana na watu wengi duniani ni ule wa yeye na rapa mwenziwe wa mjini New York Nas, ambao ulikuja kusuluhishwa mnamo mwaka wa 2005. Pia mwanzoni mwa miaka ya 1990 aligombana na LL Cool J. Katika muziki wake ameshirikiana na wasanii wengine kama DMX na Ja Rule.
Tags