Mgombea Urais: Kuondoka kwa Messi Sio Mwisho wa Dunia



MGOMBEA urais katika Klabu ya Barcelona, Toni Freixa amemjia juu staa wa timu yake, Lionel Messi kwa kusema amekosa heshima kwa klabu hiyo kutokana na kitendo chake cha kuomba kuondoka.

Toni Freixa, ni mkurugenzi wa zamani wa Barcelona anaamini kuondoka kwa Messi siyo mwisho wa dunia.

Messi ameomba kuondoka hali ambayo imemuweka kwenye matatizo rais wa sasa wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, ambapo baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiandamana wakimtaka rais huyo kujiuzulu.



“Sipingi Messi kuondoka, kinachonishanga ni njia aliyotumia siyo ya heshima. Mkataba upo na unatakiwa kufuatwa, alipe euro 700m kisha aondoke,” alisema Freixa.

BARCELONA, Hispania
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad