Japan inafanya kumbukumbu ya miaka 75 tangu Marekani ilipofanya shambulio la kwanza duniani la bomu la atomic katika mji wa Hiroshima, na kufuatiwa siku tatu baadaye na bomu la pili na la mwisho katika mji wa Nagasaki, yakiuwa watu, kuvunja majengo na uwezo wa kivita wa Japan.
Kizazi cha mwisho cha walionusurika shambulio hilo kinafanyakazi kuhakikisha ujumbe wao unaendelea kuishi hata baada ya wao.
Hibakushi, ikiwa na maana watu walionusurika na bomu hilo, kwa miongo kadhaa wamekuwa sauti ya kutaka kuzuiwa kabisa kwa silaha za kinyuklia.
Kuna watu wanaokadiriwa kufikia 136,700 ambao bado wako hai, wengi wao walikuwa watoto ama hawajazaliwa katika wakati wa mashambulio hayo.
Shambulio dhidi ya mji wa Nagasaki liliwauwa watu 74,000 na mji wa Hiroshima siku tatu baadaye, liliwauwa watu 140,000.