Michelle Obama: Donald Trump sio rais sahihi kwa nchi yetu
0
August 18, 2020
Michelle Obama amemshambulia kwa maneno Rais wa Marekani Donald Trump wakati chama cha Democrats kimeanza rasmi kampeni yake ambapo Joe Biden ndiye aliyetwikwa jukumu la kuwa mgombea wa chama hicho kuelekea Ikulu.
“Donald Trump sio rais sahihi kwa nchi yetu,” amesema aliyekuwa mama taifa wa Marekani katika ujumbe wake wenye hisia uliorekodiwa wakati wa mkutano chama cha Democratic.
Waasi wa chama cha Trump cha Republican pia nao hawakusita kutoa yaliyo moyoni wakati wa mkutano huo.
Bwana Trump ambaye yuko nyuma ya Biden katika kura ya maoni, Michelle amesema.
Kwasababu ya mlipuko wa virusi vya corona, Democrats ilifutilia mbali mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika na shughuli zingine zote za kisiasa huko, Milwaukee, Wisconsin.
Lakini bado hijafahamika ikiwa mikutano hiyo kwa njia ya mtandao ambayo hotuba zake zimerekodiwa na bila uwepo wa watu wanaoshuhudia moja kwa moja kunaweza kusababisha msisimko ule ule kama ya wakati wa kabla ya janga la corona.
Chama cha Republican kitakumbana na changamoto hiyo hiyo wakati wanathibitishia umma umuhimu wao wa kuwa uongozini katika kipindi cha miaka minne kwenye mkutano wao uliopangwa kufanyika wiki ijayo.
Michelle Obama amesema nini?
Bi. Obama ambaye hotuba yake ilikuwa imerekodiwa kabla ya Bwana Biden kutangaza mgombea mwenza, Seneta Kamala Harris, siku sita zilizopita, alianza kwa kumshambulia Bwana Trump kwa maneno.
“Huwezi kudanganya mienendo yako unapofanya kazi,” alisema hivyo kwenye hotuba yake ambayo ilifunga siku ya kwanza ya mkutano wa chama cha Democrats Jumamosi.
Msemaji huyo mkuu wa siku aliongeza: “Uchumi wetu unadidimia kwasababu ya virusi ambayo huyu rais alivipuuza kwa muda mrefu.”
“Kuema ukweli ulio wazi kwamba maisha ya mtu mweusi ni muhimu bado ni jambo linalofanyiwa dhihaka katika ofisi ya juu,” Bi. Obama ameendelea kusema.
“Kwasababu kila tunapogeukia Ikulu kwa uongozi, au kutaka kupata faraja, au kupata nguvu ya uimara, badala yake tunachopata ni ghasia, mgawanyiko na ukosefu wa uelewa kabisa.”
Michelle Obama
Amesema miaka minne iliyopita imekuwa na changamoto nyingi sana kujieleza kwa watoto wa Marekani.
“Wanaona viongozi wetu wakiita wengine maadui wa serikali, na kuhamasisha dhana ya kuwa mtu mweupe ni bora.
“Wanaangalia kwa hofu wakati watoto wanapotenganishwa na familia wanapotupwa kizimbani, kurushiwa maji ya kuwasha na mabomu ya rashasha yanatumiwa katika maandamano ya amani kwasababu tu ya nafasi ya kutaka kupiga picha.”
Bi. Obama aliendelea: “Donald Trump rais stahiki kwa nchi yetu. Amekuwa na wakati mwingi sana kujidhihirisha kwamba anaweza kufanya kazi hii, lakini ni wazi kwamba mambo yamemzidi unga.
“Hawezi kuwa yule mtu ambaye sisi tunamtaka awe kwa ajili yetu.”Hivyo ndivyo ilivyo.”
Amemuelezea Bwana Biden kama “mtu mwenye heshima”, na kuzungumzia uzoefu wa mgombea wa chama cha Democratic akiwa makamu wa rais chini ya utawala wa mume wake, Rais Barack Obama.
“Hatuna budi zaidi ya kumpigia kura Joe Biden kama vile maisha yetu yanavyotegemea hilo,” alisema hivyo akiwa amevalia mkufu ulioandikwa “Piga kura”.
Rais wa Marekani, Donald Trump
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Uchambuzi na Anthony Zurcher
Wanasiasa wengine wengi wamezungumza katika mkutano wa Democratic Jumatatu usiku. Hata hivyo, aliyejitokeza kuwa na hotuba ya nguvu yenye kugusa hisia za watu ni Michelle Obama pekee.
Ukweli aliosema, ni kwamba Donald Trump hawezi kuwa yule mtu tunayemuhitaji kwa sasa”.
“Hivyo ndivyo ilivyo,” alisema, akirejelea maneno yale yale yaliyosemwa na rais hivi karibuni kuhusu kuongezeka kwa idadi ya waliokufa kwa virusi vya corona.
Hakuwa anajaribu kushawishi Rupublicans kuunga mkono upande mwingine. Hiyo ilikuwa ni kazi ya John Kasich.
Hakuwa anajaribu kushawishi watu wa mrengo wa kushoto kumuunga mkono Biden. Bernie Sanders alitatua hilo.
Bi.Obama alikuwa akizunguza na wanachama wa Democrats waaminifu, baadhi yao pengine hata wasilia majumbani, au alipigia kura chama pinzani 2016, au baadhi yao huenda ikawa mwaka huu wamekosa imani ama wameingiwa na hofu.
Lengo lake lilikuwa ni kufikisha ujumbe thabiti wenye mvuto na kutoa wito wa kuchukua hatua.
Tags