Mimi kushabikia Yanga SC sio dhambi wala siyo ugomvi- Harmonize




Msanii Harmonize amefunguka kuwa shoo yake atakayoifanya pale Uwanja wa Mkapa kwenye kilele cha Wiki ya Wananchi itakuwa shoo ya kihistoria ambayo haijawahi kufanyika nchini.



Harmonize ambaye ni CEO wa Konde Gang amesema hayo leo Jumanne, Agosti 25, 2020, akizungumza na wanahabari kwenye hafla ya uzinduzi wa msimu wa pili wa Sayona Twist ambaye yeye ndiye balozi wa kinywaji hicho.


“Watu wanauliza kwamba Harmonize ataingia pale Taifa (Uwanja wa Mkapa kwenye Tamasha la Kilele cha Wiki ya Wananchi, Yanga SC), mimi sipendi kusema maneno mengi sana, lakini hii itakuwa best performance ever.


Harmonize pia aliendelea, “Mimi kushabikia Yanga SC sio dhambi wala siyo ugomvi, na siamini kama mtu akishabikia timu flani itampunguzia mashabiki, nachofanahamu michezo si uadui, ni furaha na urafiki, lakini muziki ni biashara, wakati mwingine hizi ni mentality tu za watu, mimi sifanyi kushindana na mtu.” amesema Harmonize.


Ikumbukwe, kilele cha Wiki ya Wananchi kinatarajiwa kuwa Agosti 30, Uwanja wa Mkapa na Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Eaglenor ya Burundi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad