Minu: Nitakuwa Mjinga Nisipomuoa Snura


Mpenzi wa mwanamuziki wa Singeli nchini, Snura Mushi, Minhal azad ‘Minu’ amesema kuwa hatakuwa mjinga aliyepitiliza kama atamuoa mpenzi wake huyo kwasababu ni mwanamke mwenye busara na anafaa kuwa mama wa familia yake.

Akizungumza na Risasi Jumatano, Minu alisema kuwa tanu ameanza uhusiano na Snura, ameweza kubadilisha sana maisha yake kutokana  na uelewa mkubwa wa aliokuwepo nao, tofauti kabisa na uhusiano mwingine wowote aliowahi kupitia,hivyo kwake mwanamuziki huyo anatosha.

“ Nitachekwa na kuonekana mjinga sana kama nisipofanya maamuzi sahihi ya kumuoa Snura, yaani kwangu ametosheleza kila kitu na busara zake kwangu ndio msingi mkubwa sana yaani kiufupi ni mwanamke wa kuoa” alisema Minu.

Na Imelda Mtema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad