Mke Arejesha Mifupa ya Mumewe Nyumbani...Yagunduliwa Kwenye Mizigo ya Ndege



Polisi katika uwanja wa ndege wa Munich nchini Ujerumani wamepigwa na mshangao mkubwa wakati wakichunguza sanduku la mbao lililokuwa linasafirishwa na abiria mmoja mwenye umri wa miaka 74 ambalo waligundua kuwa lina mifupa ya mume wa mama huyo, maafisa wamesema leo.

Maafisa wa forodha, daktari na waendesha mashitaka waliitwa, na kugundua kuwa hakuna uhalifu uliofanyika, shirika la habari la Ujerumani dpa limeripoti.

Baada ya kumhoji mwanamke huyo na mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 52, polisi iligundua kuwa wanawake hao wawili walikuwa safarini kutoka Ugiriki kwenda katika nchi walikozaliwa ya Armenia kupitia Munich na Kiev.

Polisi wamesema Mama huyo alisema mume wake alifariki mwaka 2008 na alizikwa mjini Thessaloniki, Ugiriki na kwamba yeye na mtoto wake wa kike waliamua kurejesha mabaki hayo nyumbani nchini Armenia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad