No title



Mmiliki mkubwa wa vyombo vya habari mjini Hong Kong, ambaye pia ni mkoasoaji mkubwa wa China, Jimmy Lai amekamatwa mapema leo chini ya sheria mpya ya usalama kwa madai ya kushirikiana na mataifa ya kigeni, na kuchochea hatua kali dhidi ya wanaounga mkono demokrasia. 


Mwanasheria wake Mark Simon ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Lai amekamatwa nyumbani kwake majira ya saa moja za asubuhi, na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake ya Next Digital pia wamekamatwa. 


Chanzo cha kipolisi kilichozungumza kwa sharti la kutotaja jina kililiambia AFP kwamba Lai alikamatwa kwa madai ya kushirikiana na mataifa ya kigeni na udanganyifu. 


Lai anamiliki gazeti la kila siku la Apple Daily na jarida la Next, ambayo kwa uwazi yanaunga mkono demokrasia kuikosoa vikali Beijing. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad