Ndege kutoka nchini Uturuki ilio na msaada wa vifaa vya matibabu na mdawa wawsili nchini Lebanon ikiwa ni moja ya hatua ya ushirikiano baada ya mji huo kukumbwa na jali ya moto uliotokea katika bandari ya Beyruth.
Watu zaidi ya 130 wamefariki katika mlipuko huo uliotokea mjini humo Agosti 4.
Wauguzi na wataalamu wa afya katika matukio ya dharura 21 kutoka Uturuki wamewasili pia mjini Beyruth.
Maafisa wa shirika la AFAD na Kızılay ni miongoni mwa watu waliosafiri na ndege hiyo kuelekea nchini Lebanon.
Wizara ya ulinzi ya Uturuki kupitia ukurasa wake wa Twitter imepeperusha ujumbe wa pole na kufahamisha kwamba ndege ilio na msaada wa madawa imewasili mjini Beyruth.
Safari ya ndege hiyo ilianzia uwanja wa ndege wa jeshi mjini Ankara.