Mtu mmoja auawa na 2 kujeruhiwa katika ghasia za Wisconsin



Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili kujeruhiwa katika mji wa Kenosha nchini Marekani jana usiku, wakati wa ghasia zilizozuka kwenye maandamano juu ya mauaji ya Mmarekani mweusi yaliyofanywa na polisi. 


Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakikimbia katika mitaa ya mji wa Kenosha huko Wisconsin huku milio ya risasi ikisikika, na vidio zikionyesha baadhi ya watu waliojeruhiwa wakiwa wamelala chini. 


Ghasia hizo zimetokea wakati mamia ya waandamanaji walipoandamana kwa usiku wa tatu kufuatia mauaji ya Jacob Blake, aliyeonekana kwenye vidio akipigwa risasi mara tatu na afisa wa polisi mjini Kenosha siku ya Jumapili. 


Blake alikuwa akijaribu kuingia kwenye gari akiwa na watoto wake watatu ndani wakati alipopigwa risasi. Ripoti za vyombo vya habari zinasema baadhi ya raia walionekana na silaha usiku wa Jumanne. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad