Mtu wa kwanza kupandikiza uso afariki dunia Marekani
Connie Culp, mtu wa kwanza kupandikiza uso nchini Marekani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 57.
Culp anasemekana kuwa alipoteza maisha siku ya Jumatano kutokana na maambukizi ambayo hayakuhusiana na oparesheni ya kupandikiza uso wake.
Culp, ambaye sehemu ya kati ya uso wake iliharibiwa baada ya kupigwa na mmewe mnamo 2004, alifanyiwa upasuaji wa masaa 22 mnamo 2008.
Akiongea na wanahabari kuhusu upasuaji wake, Culp alisema alikuwa na furaha na kupandikiza uso,
"Ninaweza kuvuta harufu sasa. Naweza kula nyama, naweza kula karibu chakula chochote kigumu. Kwa hivyo kila kitu kinaendelea kuwa bora. " alisema mwanamke huyo.