Kitendo cha kukamatwa kwa Yassin Juma kililaaniwa dunianiImage caption: Kitendo cha kukamatwa kwa Yassin Juma kililaaniwa duniani
Mwandishi wabari wa Kenya Yassin Juma ameachiliwa huru kutoka mahabusu nchini Ethiopia – takriban wiki moja baada ya wakili wake kusema kuwa alipatwa na maambukizi ya virusi vya corona gerezani.
Amehamishiwa kwenye hospitali ya serikali kwa ajili ya matibabu, na ataruhusiwa kusafiri kurejea nyumbani Kenya baada ya kupona.
Bwana Juma,ambaye ni mwandishi huru wa habari, alikamatwa katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, mwezi wa Julai, kufuatia ghasia zilizoibuka baada ya kuuawa kwa mwanamuziki maarufu wa jamii ya Oromo Hachalu Hundessa
Maafisa nchini Ethiopia wiki hii waliamuru kuachiliwa kwake, wakisema “alikamatwa kimakosa”.
Wizara ya Mambo ya nje ya Kenya ilisema kuwa aliachiliwa baada ya ubalozi wake nchini Ethiopia kuingilia kati na ambao ulipinga kushikiliwa kwake.