Naibu Waziri Kanyasu: Kuleni Nyama ya Mamba ni Tamu



NAIBU Waziri wa  Maliasilia na Utalii, Constantine John Kanyasu amesema kuwa Mamba ana nyama tamu na ngozi yake ni biashara nzuri huku akiwataka wanaohitaji kuvuna Mamba kuomba vibali kwa Maafisa wanyamapori.

“Mamba ana nyama tamu sana, anzeni kula nyama yake badala ya kutegemea kitoweo cha samaki pekee” amesema Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu.

Amesema kuwa licha ya nyama hiyo kuwa tamu, lakini kwanza mvunaji wa mamba aombe kibali kutoka kwa maofisa wanyamapori cha kuwavuna kinachotolewa kila Julai Mosi.

“Kuacha nyama yake kuwa tamu, lakini pia ngozi yake ni biashara yenye tija ndani na nje ya nchi,” amesema. Aidha, Kanyasu ameeleza kuwa Serikali ina mpango wa kufungua mabucha yatakayouza nyama za wanyamapori katika maeneo mbalimbali nchini.

“Wizara imeanzisha utaratibu wa uwindaji wa ndani (resident hunting) ambapo nyama zitakazo kuwa zikipatikana zitakuwa zikiuzwa kwenye mabucha hayo,” amesema.

Amesema hiyo itasaidia wananchi kupata nyama za pori kwa urahisi pale wanapokuwa na uhitaji. “Hivyo wawindaji watatakiwa kufuata taratibu za kuomba vibali kwa ajili ya kuwinda ambavyo vitaainisha aina ya wanyama ambao watakwenda kuwawinda.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad