Ndege ya Jeshi la Kenya Laanguka Somalia, Habari Tatanishi Zaibuka


Ndege hiyo likuwa ikirejea Kenya baada ya kupeleka vifaa kwa AMISOM. Picha: Hisani

Ndege hiyo ya kijeshi ilianguka eneo la Dhobley, Lower Juba

likuwa ikirejea Kenya baada ya kupeleka vifaa kwa AMISOM

Abiria saba waliokuwa ndani ya ndege hiyo walipata majeraha akiwemo rubani

Ndege moja ya kijeshi imeripotiwa kuanguka nchini Somalia katika eneo la Dhobley, Lower Juba Jumatatu, Agosti 3.

Kulingana na habari iliyochapishwa na jarida la Nairobian, ndege hiyo ilikuwa safarini kurejea Kenya  baada ya kupeleke vifaa kwa AMISOM ajali hiyo ilipotokea.

Imebainika kuwa abiria saba waliokuwa kwenye ndege hiyo walijeruhiwa akiwemo rubani, wawatu wakisafirishwa kwa ndege upesi hadi Nairobi kwa matibabu ya dharura.

Wengine wanne waliokuwa na majeraha madogo madogo walitibiwa katika hospitali ya kambi ya AMISOM iliyoko Dhobley.


Elikopta ya jeshi la Kenya. Picha:Hisani

Hadi wakati chapisho hili linapokwenda hewani, makao makuu ya AMISOM halijatoa taarifa kuhusiana na ajali hiyo habari kinzani zikiripotiwa na vyombo va habari vya Somalia baadhi vikieleza kuwa mmoja alifariki.

Hii ni ndege ya pili ya jeshi la Kenya kuanguka chini ya mwezi mmoja, nyingine ikianguka mapema Jumatatu , Julai 13 katika eneo la Kanyinga, Kithyoko kaunti ndogo ya Machakos.

Visa vya ndege za Kenya kuanguka nchini Somalia vimepanda moja ikianguka Beledweyne Jumanne, Julai 14 baada ya kujaribu kuzuia kugonga punda wakati wa kutua.

Ndege nyingine ya Kenya ilitua ghafla Somalia katika eneo la Badere, Gedo Jumapili, Julai 5 katika hali tatanishi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad