Ndege ya Kenya Yazuiwa kutua Somalia, Habari Kamili


Hatua hiyo inajiri saa chache baada ya Somali kufungua anga kwa safari za kimataifa. Picha: hisani

Ndege hiyo ilidaiwa kukiuka kanuni zilizowekwa kukabiliana na covid19

Ndege hiyo ilibeba tani 11 ya miraa

Hatua hiyo inajiri saa chache baada ya Somali kufungua anga kwa safari za kimataifa

Somalia ilipiga marufuku utumiaji wa miraa nchini kuzuia maambukizi ya corona

Kenya imepata pigo baada ya ndege yake moja kuzuiwa kutua nchini Somalia saa chache tu baada ya safari za kimataifa kufunguliwa tena Jumatatu, Agosti 3.

Kulingana na jarida la TUKO.co.ke, ndege hiyo ilikuwa imebeba tani 11 ya miraa kupeleka nchini humo.

Inadaiwa kuwa ndege hiyo ilizuiliwa kutua nchini humo baada ya kukiuka kanuni zilizowekwa na serikali ya Somalia kama njia ya kuzuia kusaamba kwa maambukizi ya virusi hatari vya corona.

Kenyan DHC-8 carrying aid crashes in Somalia

Somalia ilisitisha biashara ya miraa mwezi Machi kama njia ya kuzui kusambaa virusi vya corona. Picha: Hisani

Somalia ilichukua hatua ya kupiga marufuku matumizi ya miraa Machi, 2020 wiki chache tu baada ya virusi vya corona kulipuka nchini humo.

Hii si mara ya kwanza ambapo ndege ya Kenya inazuiwa kutua Somalia, ndege nyingine iliyobeba tani 13 ya miraa ilizuiwa kutua humo Machi.

Wakulima wa miraa katika eneo la nyambene kupitia kwa mwenyekiti wao Kimathi Munjuru wameilaumu vikali serikali ya Kenya kwa kukosa kuweka mkataba na Somalia kuhusu biashara ya bidhaa hiyo.

Kulingana na Munjuru, ndege hiyo iliyozuiwa kutua Somalia iliambatana na kukamilisha kanuni zote kuhusiana na COVID19.

Somalia ilisitisha biashara ya miraa mwezi Machi kama njia ya kuzui kusambaa virusi vya corona

Haya yanajiri siku chache tu baada ya Kenya kuifungia ndege za Tanzania anga serikali ya Tanzania ikichukua hatua sawa kama kisasi.

Nchi hizo mbili zililazimika kuafikia mkataba wa kufunguliana anga baada ya majadiliano.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad