Ndugai ataka Wabunge wa CCM wawe wengi zaidi


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai, amesema kuwa demokarsia ya kibunge siyo suala la Mbunge kuwa na ujuzi wa kuzungumza bali ni uwezo wa Wabunge kufanya maamuzi, hivyo amewataka Wabunge wa CCM wawe wengi zaidi kuliko wa vyama vingine ili waweze kufanya maamuzi.


Ndugai ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 29, 20202, wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM, uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, ambapo pia ameongeza kwa kuwa tayari kuna Wabunge na Madiwani ambao wamepitishwa bila kupingwa hivyo kazi kubwa iliyopo ni ya kumnadi mgombea Urais pekee kupitia chama hicho Dkt Magufuli.

"Mimi kama Spika katika demokrasia ya kibunge suala siyo ujuzi wa kuzungumza na kupanga hoja, umuhimu ni uwezo wa kuamua, ni muhimu sana Wabunge wa CCM wakazidi theluthi mbili za Wabunge wote, ili tuweze kuamua jambo lolote linaloletwa Bungeni na Serikali yetu", amesema Spika Ndugai.

Aidha Ndugai ameongeza kuwa, "Ndugu zangu wana Dodoma tunayo kila sababu ya kumchagua Magufuli kampeni yetu ya safari hii kwa sababu Madiwani wengi wamepita bila kupingwa na baadhi ya majimbo Wabunge wamepita moja kwa moja iwe ya Rais tu na iwe ya Nyumba kwa Nyumba".

Mbali na hayo Ndugai amesema kuwa, mpaka sasa maandalizi ya Bunge la 12 yamekamilika kwa asilimia 82, na kwamba Bunge la 12 litakuwa ni la kisasa zaidi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad