Newcastle kuuzwa kwa Matajiri wa Singapore


Baada ya timu ya Newcastle kushindwa kuuzwa kwa mfanyabiashara kutoka familia ya kifalme ya Saudi Arabia, kutokana na kile kilichoelezwa historia ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu toka katika familia hiyo ya kifalme katika utawala wake


 Mike Ashley ambaye ndiyo  Mmilikiwa timu hiyo mwishoni mwa mwaka  2017 alitangaza kuiweka sokoni timu yake ilikupata  Mmiliki mwingine bila mafanikio hadi mwaka  2020 alipojitokeza Mfanyabiashara Prince Mohamed  bin Salmin kutoka Saudi Arabia akisaidiwa na   Amanda  Staveley  Mwanamke shujaa katika biashara ya soka, Kwani ndiyo aliyefanikisha dili ya kuuzwa kwa Manchester City

Baada ya kushindikana kwa mpango  huu kwa upande wa Mwana wa mfalme Mohamed  bin Salmin ni kama walikata tamaa hadi ilipojitokeza kampuni nyingine Bellagraph Nova Group (BNG) ya Singapore ambaye huwenda akafanikiwa kwa kuwa hana  kashfa zinazoweza kuzuia ununuzi huu kufanyika

Kama mpango huu utafanikiwa basi huwenda ukaongeza ushindani mkubwa kwenye  ligi ya  ya England kama ilivyokuwa kwa  Chelsea na Manchester City kufanya  mapinduzi makubwa ya kiushindani baada ya kununuliwa na  Matajiri wa Mataifa mengine
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad