Ni Kweli Roho ya Binadamu Ina Uzito wa Gramu 21?



WATU wa kale nchini Misri walikuwa wakisema kwamba  baada ya kifo binadamu huingia katika safari ndefu yenye matatizo hadi pale tunapowasili katika ukumbi ambao roho uhukumiwa.

Kilele chake ni wakati roho ambayo mambo yote mazuri na mabaya husajiliwa na hupimwa katika mzani. Iwapo mtu ameishi maisha mema, roho zetu zitakuwa na uzito sawa na ule wa manyoya na kwamba utaishi milele peponi.

Habari kama hizo zilichapishwa katika jarida la tiba la Marekani  na lile la Kijamii la Utafiti wa kisaikolojia 1907 chini ya kichwa cha habari cha ‘Roho’  na ushahidi wa majaribio ya uwepo wake.

Kichwa cha gazeti la The New York Times ambalo liliandika habari hiyo kilikuwa wazi kwamba roho ina uzani, kulingana na daktari.

Daktari aliyenukuliwa alikuwa Dancan McDougall, aliyezaliwa mjini Glasgow, Uskochi 1866, na kuhamia mjini Massachusets, nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 20 baada ya kujipatia shahada yake katika chuo kikuu cha tiba mjini Boston.

Kama mtaalamu alihudumu muda wake mwingi kusaidia hospitali za hisani za wagonjwa wasiotibika katika mji wa Havernhill.

Kulingana na taarifa iliochapishwa na gazeti la The New York Times miaka sita iliopita, lengo lake ilikuwa kuchunguza iwapo kuondoka kwa roho katika mwili wa mwanadamu kulikuwa kunaweza kuambatana na dhihirisho lolote ambalo linaweza kusajiliwa. Ingawa lengo lake halikuwa kubwa kama lile la miungu ya Wamisri, Utafiti wake ulikuwa muhimu.

Utagundua kwamba alianza kwa kusema kwamba roho inamuondokea mwandamu anapofariki, hivyo basi hakutaka kujua uwepo wake, lakini matokeo ya utafiti wake yalikuwa na uwezo kudhihirisha kisayansi hata iwapo hilo halikuwa lengo lake.

MacDougal alijenga kitanda maalum alichoweka mzani

Katika kitanda hicho wagonjwa mahututi walio katika hatua yao ya kufariki walilazwa na kuchunguzwa wakati wa kifo chao na baadaye. Mabadiliko yoyote yanayohusiana na uzani yalipimwa, yakitilia maanani maji ya mwilini, kama vile joto, haja ndogo na gesi kama vile oksijeni na Nitrojen.

Akishirikiana na watalaamu wengine kila mmoja wao akifanya hesabu zake, iligunduliwa kwamba  kulingana na MacDougal kwamba uzani wa kati ya gramu 14 hadi 35 hupungua katika mwili wa mwanadamu wakati anapofariki. Uzani upande mmoja ulianguka kwa kasi, kana kwamba kitu kilikuwa kimetoka katika mwili, alisema daktari huyo.

MacDougal pia alifanya majaribio kama hayo na mbwa 15 na kubaini kwamba matokeo yake yalikuwa tofauti, hakukuwa na upungufu wa uzani wakati wa kifo, ili kuunga mkono nadharia kwamba upungufu wa uzani ulioonekana katika mwili wa mwandamu ulikuwa unahusishwa na roho kuondoka katika mwili, kutokana na imani kwamba kulingana na dini yao wanyama hawana roho.

Tatizo la utafiti wake uliochukua miaka sita ni kwamba ulikuwa ukitegemea idadi ya visa sita pekee. Zaidi ni kwamba visa viwili havikuweza kutiliwa maanani, kimoja kwasababu ratili yake haikuweza kubadilishwa ili kupima uzani uliostahili mbali na kwamba watu waliokuwa wakipinga utafiti wake waliingilia kazi yake

”Sababu nyengine ni kwamba hayakuwa majaribio ya sawa. Mgonjwa alifariki karibia dakika tano baada ya kulazwa kitandani na alifariki wakati nilipokuwa nikirekebisha ratili.”

Mbali na hayo matokeo yake yalitokana na majaribio ya wagonjwa wanne, ijapokuwa kati ya wagonjwa watatu kulikua na upungufu wa uzani, uzani wa wawili kati yao uliongezeka kwa muda na huku uzani wa mgonjwa wa nne ukishuka baada ya kupimwa mara ya pili.

Ijapokuwa magazeti kutoka kwa maeneo ya dini yalichukulia matokeo ya utafiti huo kuwa dhihirisho la uwepo wa roho, MacDougal mwenyewe hakushawishika kwamba kazi yake imethibitisha chochote. Kwake, ripoti yake ilikuwa tathmini ya mapema, na akasema utafiti zaidi unahitajika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad