Njombe:Bweni la wasichana lanusurika kuungua moto,laungua mara mbili



Bweni moja la wasichana wa shule ya Sekondari Maguvani halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani NJOMBE limenusurika kuungua moto usiku wa tarehe 20 majira ya saa mbili usiku.


Mkuu wa shule hiyo TUDEN MAHENGE amesema tukio hilo ni la Tatu huku likiungua mara mbili na sababu zikidaiwa ni wananchi ambao hawakuridhishwa na maamuzi ya eneo hilo kujengwa shule.


Akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na usalama Mkuu wa mkoa wa NJOMBE Mhandisi MARWA RUBIRYA amekuatana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Makambako PAUL MALALA ili kupata taarifa ya awali.


"Mimi nikiwepo hapa halmashauri ya mji ya Makambako hii ni mara ya pili,mara ya kwanza vile vilev ilitokea bweni lile lile na tuna takribani mwaka mmoja tangu tumalize ukarabati"alisema Paul Malala


Baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari MAGUVANI kamati hiyo imekagua na kushuhudia uharibifu wa samani za bweni na mali za wanafunzi.Mkuu wa shule hiyo TUDEN MAHENGEMwalim Mahenge amesema tukio hilo ni la Tatu kutokea. 


"Moto wa kwanza ulitokea machi 2018 na uliunguza jengo zima la wasichana,lakini 2018 mwezi septemba uliwaka tena kwa kuanzia juu ya kitanda cha msichana mmoja ukateketeza vitanda vitatu vya wanafunzi na godoro tatu.Na ndio hisia za moto huu awamu ya tatu uliotokea tarehe 20 saa mbili usiku wakati wanafunzi wako kwenye maandalizi ya kujisomea"alisema 


Na ndipo Mkuu wa mkoa wa NJOMBE Mhandisi MARWA RUBIRYA akavitaka vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa huo kuhakikisha wanakomesha vitendo hivyo.


"Nimeshatoa maelekezo kwa kamanda wa polisi wa mkoa wafanye upelelzi wa kina kuhakikisha wote waliohusika wanakamatwa na wanafikishwa kwenye vyombo vy sheria"alisema Rubirya

 

Kamanda wa Polisi mkoa huo HAMIS ISSAH ameshauri wakuu wa shule kuandaa utaratibu wa kujilinda huku jeshi hilo likitoa msaada wa doria wakati wa usiku. 


Katika ajali hiyo vitanda viwili vimeungua na vitu kadhaa vya wanafunzi vikiwemo madaftari magodoro mablanketi na viatu vimeungua.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad