Ole Sendeka aaga rasmi Njombe,akabidhi ofisi kwa RC mpya



Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amewataka wataalam wa ujenzi wa barabara,madaraja na hata majengo kuacha kufanyakazi kwa mazoea kwa kuwa mkuu mpya wa mkoa aliyeletwa ni mtaalamu wa masuala hayo. 


Ole Sendeka ametoa wito huo wakati akifanya makabidhiano ya ofisi ya mkoa wa Njombe kwa mkuu mpya wa mkoa huo na kwamba yeye alifanyakazi kwa kuuliza wataalamu kwenye mambo ya kitaalamu kama ya ujenzi lakini sio mkuu wa mkoa wa sasa. 


“Kwa hiyo mmeletewa Injinia,huyu hamtacheza naye iwe bara bara za TARURA za TANROADS uwe ujenzi wa majengo yeyote huyu hamtamdanganya”Alisema Ole Sendeka 


Pamoja na mambo mengine Ole Sendeka amekabidhi hundi ya zaidi ya shilingi Bilioni tano ambazo ni fedha zilizookolewa toka kwa watu wachache waliofuja fedha za iliyokuwa benki ya wananchi Njombe Njocoba na vyama vya ushirika. 


“Hi ni hundi ya shilingi bilioni 5.397 ya fedha za wananchi ambazo zimerejeshwa baada ya Rais Dkt,John Pombe Magufuli kwamba wakuu wa miko na wakuu wa wilaya kuhakikisha wale wote waliochukuwa fedha za vyama vya ushirika,vyama vya msingi na SACCOSS wanazirudisha,na leo namkabidhi mkuu wa mkoa wa Njombe ili akaweka utaratibu wa kuzigawa fedha hizi”aliongeza Sendeka 


Awali katibu tawala mkoa wa Njombe Catalina Revocati amesema kuwa Ole Sendeka enzi za utawala wake alikuwa kiongozi wa mfano kwa kuwa aliweza kuwaongoza watendaji wake wote kwa kuzingatia maelekezo yake anayoyatoa na kuyafanyia kazi kikamilifu. 


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi ya mkoa mkuu mpya wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Mwita Rubirya amesema anatarajia kuona viongozi wa ngazi za wilaya na halmashauri wanakuwa  wa kwanza kutatua changamoto za wananchi kabla hazijamfikia yeye kama kiongozi mkuu wa mkoa. 


“Tuna wajibu mkubwa kuhakikisha tunasaidia wananchi katika kutatua kero zao,mwananchi anaposhindwa kutatuliwa kero zake hakika anasononeka,sasa nitashangaa kuona kuwa kuna kero ambazo zimetokea katika wilaya Fulani mpaka anayelalamika aipeleke kwenye mamlaka za juu”alisema Rubirya 


Mhandisi Rubirya aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe mara baada ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo kwenda katika majukumu mengine ya kisiasa 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad