Polepole Awaka ”CHADEMA waombe radhi kubadili wimbo wa Taifa”
0
August 06, 2020
Katibu wa uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Humprey Polepole ameshangazwa na kitendo cha chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kubadilisha beti kwenye wimbo wa taifa wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 5, 2020 Jijini Dar es Salaam katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba amesema kitendo cha chama hicho kubadilisha nyimbo hiyo ni kuvunja sheria.
“Hiki nichama ambacho kabla hakijapata dola kinaanza kubadilisha wimbo wa watanzania kuwa wimbo wa chama chao, tena kwa kujimwambafai kuwa wako sahihi, huu ni wimbo unowatambulisha watanzania sio wimbo unaotambulisha chama cha mtu fulani” amesema Polepole.
“Mimi hiki Chama nimeshindwa kukielewa, nidhamu ni zero, kutii sheria bila shuruti ni zero, kama haikutosha ikaja ya wimbo wa Taifa, bila aibu wanajenga hoja tuambieni wapi tunavunja sheria”amesema Polepole
Tags