Polepole: CHADEMA Imemdhulumu TID ‘Ni Yeye’




KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamemzulumu mwanamuziki TID kwa kutumia kaulimbiu aliyoibuni ‘Ni Yeye’ bila kumshirikisha.


 


Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Humphrey Polepole ameeleza kuwa kitendo hicho hakikubali na kwamba Watanzania watakichukulia hatua chama hicho cha upinzani.


 


“Nampa pole TID sababu hawa majamaa ni mazulumati wametudhulumu wimbo wa Taifa. TID anapambana mtu wa watu ametengeneza Ni Yeye na ile ilikuwa Magufuli, wale majamaa wameichomeka kule. Hawajamshirikisha hawajamuomba kwa kweli sisi kama Watanzania tutawachukulia hatua,” ameeeleza Polepole.


 


Katika hatua nyingine ameeleza kuwa Rais Dkt. Magufuli ambaye ni mgombea wa CCM atachukua fomu ya uteuzi wa kugombea Urais wa Tanzania wiki hii jijini Dodoma, lakini hakutaja siku ya tukio hilo.


 


Aidha, amesema Agosti 15 mwaka huu chama hicho kitakutana na wasanii zaidi ya 109 pamoja na bendi katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kutambulisha nyimbo zitakazotumika kabla, wakati na baada ya kampeni.


 


View this post on Instagram

 


Msanii wa muziki tidmusic amewasilisha malalamiko yake kupitia ukurasa wake wa Instagram akidai kutofurahishwa na kinachoendelea mitandaoni baada ya baadhi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutumia msemo ya’NI-YEYE’ kwa Tundu Lissu wakati wa mkutano mkuu wa kumpitisha mgombea Urais wa chama hicho kwenye uchaguzi mkuu 2020. TID amedai kuwa CHADEMA hawajafanya mazungumzo yoyote juu ya kutumia msemo huo kwenye kampeni zao, na kitendo cha wao kuutumia bila makubaliano ni kitu kinachomuumiza sana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad