Rais Magufuli Kuchukua Fomu Leo
0
August 06, 2020
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Magufuli, leo Tarehe 06 Agosti, 2020 atachukua fomu ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya UchaguziTanzania (NEC) Njedengwa Jijini Dodoma.
Rais Magufuli atachukua fomu majira ya Saa tatu asubuhi na atasindikizwa na watu wachache wakiwemo viongozi wakuu wa Chama, ikiwa ni kutekeleza matakwa na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Rais Magufuli anachukua fomu hiyo ili kugombea Urais kwa kipindi cha Pili katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.
Baada ya kuchukua fomu, Rais Magufuli atakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma (White House) ambako atakutana na wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM na kuwasalimu.
Tags