Rais Putin wa Urusi atangaza chanjo ya kwanza ya corora duniani



Rais Vladmir Putin wa Russia ametangaza leo kuwa, nchi yake imetengeneza chanjo ya kwanza kabisa ya virusii vya corona inayotoa kinga ya kudumu dhidi ya virusi hivyo.


Rais Vladimir Putin amesema kuwa tayari binti yake mmoja amepewa chanjo hiyo inayozuia kuambukizwa virusi vya corona na maradhi ya COVID-19.


Televisheni ya Russia Today imeripoti kuwa, Putin amesema katika mazungumzo yake ya mawaziri wa serikali ya Moscow kwamba: "Mapema leo na kwa mara ya kwanza kabisa duniani, tumesajili chanjo ya kwanza dhidi ya virusi vya corona nchini Russia."  


Rais wa Russia amesema kuwa chanjo hiyo imevuka awamu zote za majaribio.


Wiki kadhaa zilizopita Naibu Waziri wa Afya wa Russia, Olek Grenev alikuwa ametangaza kuwa, chanjo hiyo imeingia katika majaribio ya mwisho.


Vilevile mwezi uliopita afisa mmoja wa ngazi za juu wa Wizara ya Afya ya Russia alitangaza kuwa inatarajiwa kwamba chanjo ya virusi vya corona itaanza kuzalishwa kwa wingi nchini humo mwezi Septemba mwaka huu. 


Credit:Parstoday


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad