Rais Donald Trump wa Marekani ameelek mji wa Kenosha, jimboni Wisconsin, ambako kumekuwa na vurugu tangu ofisa wa polisi alipomfyatulia risasi mgongoni Mmarekani mweusi.
Rais Trump aliyasema hayo mjini Texas, baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kama anawezea kwenda katika mji huo, ambao afisa wa polisi alimfyatulia risasi Jacob Blake ambae kwa hivi sasa anapatiwa matibabu baada ya kupooza sehemu yake ya chini ya mwili kuanzia kiunoni kutokana na kushambuliwa kwa risasi.
Kijana wa umri wa miaka 17 anashikiliwa na mamlaka ya Kenosha kwa kuhusishwa na mashashambulizi watu watatu waliokuwa wakiandamana kupinga shambulizi la Blake, ambapo wawili miongoni mwa hao walipoteza maisha.
Hata hivyo Trump ambae ambae alikuwa mjini Texas kwa ajili ya kutathimni athari za kimbunga Laura, hakutoa ufafanuzi zaidi kuhusu safari yake hiyo.