Rais wa Lebanon Agoma Kujiuzulu



Rais wa Lebaon, Michel Aoun amesema uchunguzi kuhusu mlipuko mkubwa uliotokea mapema mwezi huu mjini Beirut na kuwaua Watu zaidi ya 180 na kujeruhi maelfu wengine ni mgumu na huenda hautokamilika haraka.
Auon amesema uchunguzi huo umegawanywa kwenye hatua tatu na utahitaji muda zaidi kuweza kubaini kikamilifu kilichotokea kabla ya kufikia hitimisho.

Akijibu kuhusu shinikizo la kumtaka kujiuzulu kutokana na madai ya uzembe, Aoun amesema suala hilo haliwezekani kwa sababu litaacha ombwe la uongozi nchini humo.

Hadi sasa chanzo cha moto uliozuka kwenye ghala lililohifadhi maelfu ya tani za milipuko katika bandari ya Beirut bado hakijulikani.

Duru kutoka Lebanon zinasema viongozi wa juu wa Nchi hiyo akiwemo Rais Aoun walifahamu uwepo wa hifadhi hiyo ya milipuko lakini hawakuchukua hatua.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad