Rais wa Uganda Yoweri Museveni atangaza maombi kwa ajili ya corona



Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza Jumamosi kuwa siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya Covid-19.

Rais huy amesema kuwa alipata wazo kutoka kwa raia wa Ugandaambaye alikuwa na “maono kutoka kwa Mungu “.


“Mungu alikua amemuambia katika moano kwamba ninapaswa kuanda maombi, yaandaliwe kisayansi, ili Mungu atuponye na Covid-19…Ninatangaza tarehe 29 Agosti, 2020, siku ya maombi ya kitaifa na siku ya mapumziko ya umma. Kaeni majumbani mwenu au kwenye viwanja vya nyumba zenu na muombe,” Bwana Museveni alisema katika ujumbe wake wa mtandao wa kijamii.


Hadi sasa Uganda imerekodi watu 2,679 wenye maambukizi ya virusi vya coronana vifo 28.


Serikali iliweka masharti ya kudhibiti maambukizibaada ya kuthibitisha kisa cha kwanza mwezi Machi.


Therefore, by the powers given to the President of Uganda by Section 2(2) of the Public Holidays Act, I declare the 29th of August 2020, a day of National Prayers and a Public Holiday. Stay in your houses or Compounds and pray. pic.twitter.com/9Zl5RNnlR1


— Yoweri K Museveni (@KagutaMuseveni) August 27, 2020

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad