Ronaldinho aachiwa huru na kutoka kizuizini nchini Paraguay



Nyota wa zamani wa Brazil ,Ronaldinho Gaucho ametoka kizuizini alipokuwa anashikiliwa kwa zaidi ya miezi 5 baada ya Mahakama moja nchini Paraguay  kumuhukumu adhabu hiyo kutokana na madai ya hati bandia ya kusafiria.



Ronaldinho Gaucho akiwa mahakamani nchini Paraguay .


Gaucho ambaye ni mshindi mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora Dunia na FIFA ,ni mmoja ya wachezaji waliofanya makubwa katika soka la dunia, akitwaa tuzo mbalimbali ikiwemo kombe la dunia mwaka 2002 akiwa mchezaji kinda kabisa nyakati hizo


Staa huyo wa zamani wa vilabu vya PSG,Barcelona na hata AC Milan,likuwa anashikiliwa na mamlaka  za usalama za Paraguay pamoja na kaka yake ,Roberto de Asas ambaye anatambulika kama meneja wa nyota huyu wa zamani .


Nje ya soka Gaucho anatajwa kama mchezaji anayependa sana anasa na maisha ya ufahari yaliyochangia kutofanikiwa zaidi katika soka  na hata sakata hili la kuingia nchini Paraguay kwa hati ya bandia inaelezwa kuwa walikuwa wanakwenda katika uzinduzi wa moja ya kumbi za starehe ya usiku maarufu kama Cassino.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad