RPC Arusha awatoa hofu wananchi Kuhusu Machafuko ya Uchaguzi


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Salum Hamduni, amesema kuwa Uchaguzi Mkuu unaokuja mwezi Oktoba, utafanyika kwa uhuru na haki ili kuwafanya wananchi kuchagua viongozi wanaowataka na kwamba watasimamia kwa weledi uchaguzi huo na kufuata sheria na taratibu zilizopo.

Kamanda Hamduni ametoa kauli hiyo, wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Intelejensia ya Makosa ya Jinai Charles Mkumbo ya kupima ni kwa namna gani Jeshi hilo limejipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu.

"Niwaahidi tu wananchi wa Mkoa wa Arusha sisi tupo kwa ajili ya kusimamia haki, na uchaguzi utakuwa wa haki na tutajitahidi sana sisi kama Jeshi la Polisi tunatimiza wajibu wetu wa kuhakikisha utulivu na amani wakati wote wa uchaguzi", amesema Kamanda Hamduni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Intelejensia ya Makosa ya Jinai, Charles Mkumbo, amesema kuwa katika Uchaguzi Mkuu ujao hakuna mwananchi yeyote atakayeonewa, huku akiwataka wananchi wafuate taratibu na kanuni za uchaguzi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad