Rwanda yafunga masoko makuu baada ya ongezeko la virusi vya corona



Rwanda imefunga masoko makuu ya jijini Kigali kwa muda wa siku 7 kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya corona.

Masoko yaliyofungwa ni pamoja na soko kuu la Nyarugenge mjini Kati na soko la Nyabugogo maarufu kwa walanguzi.

Wizara ya afya imetangaza kwamba itaanzisha zoezi la kufanya vipimo vya watu kwenye masoko yanayoendelea na shughuli zake kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuchukua mikakati zaidi.

Kulingana na wizara ya afya ya Rwanda watu 151 walipatikana na virusi vya corona kufuatia sampuli zilizochukuliwa mnamo siku mbili zilizopita,wengi wao walipatikana katika masoko hayo.

Rwanda imekwisharekodi visa 2,453 vya Covid19.watu 1,648 walipona,wengine 797 bado wanapata matibabu na 8 walikufa.

Kwa upande mwingine wizara ya mambo ya ndani imesema kwamba baadhi ya masoko yatahamishiwa ya jiji la Kigali kwenye sehemu zilizo wazi ili kupunguza msongamano kwenye masoko.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad