Sababu 11 kwanini Lissu Atapata Ushindi wa Asilimia Ndogo Kuliko Wote Tangu 1995


1: JPM anamengi yakuonekana aliyofanya kwa wananchi Lissu hata jimbo lake tu hakuna chochote cha kuonyesha.

2: Kila vita anayoingia JPM anapata ushindi au nusu ushindi (MAKINIKIA) wa kugusika, Lissu ni nusu ushindi au ushindi wa maneno.

3: Lissu amejipanga kutumia tuhuma kujinadi wakati JPM atakuwa na muda wa kutangaza na kuwaonyesha watanzania aliyowafanyia.

4: Taifa bado linamwangwi wa utisho wa kazi za JPM na maamuzi magumu kama KORONA, Lissu kaanza udalali wa kutaka kutuaminisha watu wanakufa korona kipindi ambacho kila kanisa linatoa ibada za shukrani kwa Mungu kutupa rais Jasiri.

5: Wakati wananchi wanameaminishwa MABEBERU ni watu wabaya, LISSU anaonekana kutegemea watu hao ambao wapiga kura wanaamini ni wabaya kama watu wake wa karibu.

6: Tangu amepata Janga la kumiminiwa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni Risasi Kila akisimama kuongea anaongea yaleyale hadi anaboa. Wakati Tunategemea JPM atoe mambo mapya licha ya kuwa na mengi ya kusema.

7: Kanda ya ziwa huwa inaamua nani ashide uchaguzi kwa idadi kubwa ya wapiga kura, huko tumeshuhudia vitendo vingi vya maendeleo kuliko maneno ya kipinzani na malalamiko. Wanatarajia Lissu utawafanyia nini zaidi ya Meli, Busisi, Barabara, Viwanda, zahanati etc ila naona umejipanga kuwapelekea tuhuma na maneno ya kujirudiarudia.

8: Lissu maarufu mitandaoni ila katika uhalisia kwa wapiga kura Magufuli ni maarufu kuliko Lissu.

9: Lissu amekaa kama mtu anayetakiwa kusumbua mfumo sio kuwa kiongozi wa mfumo wa kuwasaidia watu. Maneno yake, Body language yake haimfanyi mpiga kura aone kuwa hapo kuna jamaa mwenye utisho wa kuwa kiongozi wa nchi. Angalau Membe kidogo.

10: Hakuna mtu wa kuvujisha taarifa za siri za kiserikali na kiCCM ili ziwape wapinzani kiki kama enzi za Dr Slaa. Karibu watu wote wanahofu hata tu kulitaja jina la JPM kimizaha. Kwa kipindi ambacho hakuwepo LISSU nchi imebadilishwa saikolojia kabisa jambo ambalo halihitaji miezi miwili kulirudisha.

11: Kwa sasa JPM haonekani kama Kiongozi wa nchi tu bali pia kama Kiongozi wa Kiroho. Kuna watu leo wanamuamini JPM kuliko hata viongozi wao wa kidini maana Alionyesha utegemezi mkubwa kwa Mungu ktk Corona kuliko hofu za viongozi wao. Sio suala la miezi miwili kumtolea mtu imani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad